• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Kitty Hawk yafanya majaribio ya teksi inayoruka nchini New Zealand

    (GMT+08:00) 2018-03-19 09:17:18

    Kampuni ya Kitty Hawk iliyowekezwa na mwanzilishi wa kampuni ya Google Bw. Larry Page imedokeza kuwa imefanya majaribio ya teksi mpya inayoruka.

    Kampuni hiyo imesema kuanzia mwezi Oktoba mwaka jana, kampuni hiyo ilianza kufanya majaribio ya teksi inayoruka iitwayo Cora nchini New Zealand. Teksi hiyo haitauzwa kwa wateja binafsi, bali itatumiwa kwa usafirishaji wa umma.

    Teksi hiyo inafanana na ndege ndogo au ndege isiyo na rubani. Kuna rafadha kadhaa kwenye mabawa yake, ambazo zinaiwezesha ndege hiyo kwenda juu na kushuka chini moja kwa moja kama helikopta, na kuruka kwenye barabara ya ndege kama ndege yenye mabawa. Teksi hiyo inaweza kuruka kwa kilomita 100 na kwa urefu wa mita 150 hadi 900 angani na kwa mwendo kasi wa kilomita 170 kwa saa.

    Kampuni hiyo imesema kuna kompyuta tatu kwenye teksi hiyo, hata kompyuta moja ikiharibika, teksi hiyo bado inaweza kuruka. Parachuti pia imewekwa kwenye teksi ili kukabiliana na hali ya dharura. Teksi hiyo inaendeshwa na software na kudhibitiwa na binadamu, hivyo hata mtu asiyeweza kuendesha ndege anaweza kuendesha teski hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako