Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye yuko ziarani nchini Cuba, amempongeza Bw. Xi Jinping kwa kuchaguliwa kuwa rais wa China.
Katika taarifa yake rais Kenyatta amesema, kuchaguliwa kwa Bw. Xi Jinping kumeonesha kuwa wananchi wa China wana imani kubwa na mtizamo wake na busara zake katika utawala wa nchi na mambo ya kimataifa. Anaamini kuwa chini ya uongozi wa rais Xi, China itapata ustawi zaidi, na kuchangia zaidi kwa ajili ya amani, utulivu na ustawi wa dunia.
Rais Kenyatta amesema katika miaka kadhaa iliyopita, uhusiano kati ya Kenya na China umepata maendeleo makubwa, na miradi muhimu ya ushirikiano ukiwemo ujenzi wa reli ya SGR imeboresha maisha ya watu wa Kenya.
Pia anatarajia kushirikiana kwa karibu zaidi na rais Xi Jinping, katika kusukuma mbele uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya Kenya na China upate mafanikio makubwa zaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |