Rais John Magufuli wa Tanzania amemtumia salamu za pongezi Bw. Xi Jinping kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa China.
Katika salamu hizo rais Magufuli amesema kuchaguliwa kwa Bw. Xi Jinping kumeonesha kuwa chama cha kikomunisti cha China na watu wa China wana imani kubwa na uwezo wake wa kutawala nchi.
Amesema anaamini kuwa Tanzania na China zitakuza ushirikiano wa kunufaishana katika nyanja mbalimbali ili kuwanufaisha zaidi watu wa pande hizo mbili.
Pia rais Magufuli amesifu mchango wa China katika kuhimiza ushirikiano kati ya Afrika na China, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Amesema ana imani kwamba bara la Afrika litatimiza maendeleo ya viwanda na kilimo, na mageuzi ya kiuchumi chini ya mfumo wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika. Pia amesema chini ya Pendekezo la Ukanda mmoja, Njia moja lililotolewa na rais Xi Jinping, dunia itaimarisha muunganyiko na biashara huria, na kutimiza maendeleo ya pamoja na usalama.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |