• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma la China waamua muundo wa baraza la serikali la China

    (GMT+08:00) 2018-03-19 11:10:10

    Mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma la China umepiga kura na kuamua Han Zheng, Sun Chunlian, Hu Chunhua, Liu He kuwa manaibu mawaziri wa baraza la serikali la China, Wei Fenghe, Wang Yong, Wang Yi, Xiao Jie na Zhao Kezhi kuwa wajumbe wa Taifa.

    Kwa mujibu wa uteuzi uliotolewa na waziri mkuu Bw. Li Keqiang, mkutano huo umepiga kura na kupitisha orodha ya mawaziri wa wizara mbalimbali, wakurugenzi wa kamati mbalimbali, mkuu wa banki kuu ya China, mkaguzi mkuu wa uhasibu na katibu mkuu, pamoja na wajumbe wakurugenzi na manaibu wao, na wajumbe wa kamati mbalimbali maalumu za Bunge la 13 la umma la China.

    Leo rais Xi Jinping wa China amesaini amri ya No, 2 ya rais kupitisha uteuzi wa mawaziri wa baraza la serikali la China pamoja na watu wengine wanaoshika nyadhifa mbalimbali kwa mujibu wa uamuzi wa mkutano.

    Baada ya ajenda mbalimbali za mkutano huo kumalizika, manaibu mawaziri, wajumbe wa taifa wameapa kwa katiba ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako