• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya vifurushi vilivyosambazwa nchini China yafikia bilioni 40 mwaka jana

    (GMT+08:00) 2018-03-19 17:57:48

    Mkurugenzi wa idara ya posta ya China Bw. Ma Junsheng leo amesema, idadi ya vifurushi vilivyosafirishwa nchini China imefikia zaidi ya bilioni 40, ambayo imechukua asilimia 40 ya soko la usambazaji wa vifurushi la dunia.

    Bw. Ma Junsheng amesema, katika miaka mitano iliyopita, sekta ya usambazaji wa vifurushi imeongezeka kwa wastani wa asilimia 40 kila mwaka. Vifurushi vingi vinatokana na biashara ya kielekitroniki, na usambazaji wa vifurushi unapunguza gharama za usafirishaji, na kuinua sifa ya matumizi. Jukwaa la umma la usambazaji wa vifurushi linahimiza zaidi maendeleo ya sekta za uzalishaji wa kisasa na kilimo cha kisasa. Katika sekta ya biashara ya kielekitroniki ya kuvuka mipaka, kila siku vifurushi karibu milioni 6 hadi 7 vimesambazwa, na idadi hiyo huenda ikaongezeka.

    Bw. Ma amesema anaamini kuwa sekta ya usambazaji wa vifurushi itapata maendeleo ya kasi katika siku za usoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako