Mkuu wa shirikisho la watu wenye ulemavu la China Bw. Lu Yong leo hapa Beijing amesema, zaidi ya asilimia 90 ya watoto wenye ulemavu wamepata elimu ya lazima nchini China.
Bw. Lu Yong amesema, watoto hao wenye umri wa chini ya miaka 6 ni milioni 1.68, ambao laki 2.2 kati yao wanatoka kwenye familia maskini. Ili kuhakikisha watoto wenye ulemavu wana haki sawa ya kupata elimu ya lazima kama watoto wa kawaida, China imerekebisha kanuni ya elimu kwa watu wenye ulemavu, na kutoa mpango wa kuboresha elimu maalumu. Aidha China pia imejenga "Big Data Database" inayofuata mfumo wa kusajili majina halisi ili kuhimiza watoto wenye ulemavu wanaotoka katika familia maskini kusoma shuleni.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |