• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Putin achaguliwa tena kuwa rais wa Russia

  (GMT+08:00) 2018-03-19 19:53:07

  Tume Kuu ya Uchaguzi ya Russia imesema, rais wa sasa wa Russia Vladmir Putin amepata asilimia 76.6 za kura baada ya asilimia 99.83 ya kura kuhesabiwa katika uchaguzi wa rais uliofanyika jana.

  Mgombea wa Chama cha Kikomunisti Paven Grudinin ambaye ni mpinzani wa karibu wa rais Putin amepata asilimia 11.9 ya kura, huku kiongozi wa Chama cha Democratic Liberal Vladmir Zhirinozsky akipata asilimia 5.66 ya kura. Idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ni karibu milioni 73.4.

  Matokeo rasmi ya uchaguzi huo wa saba kufanyika tangu Russia kutambulisha mfumo wa urais mwaka 1991, yanatazamiwa kutangazwa ndani ya siku 10.

  Wakati huohuo, rais Xi Jinping wa China amempongeza rais Putin kwa ushindi wake na kusema, ana uhakika kuwa wananchi wa Russia watapata maendeleo mapya ya taifa chini ya uongozi wa rais Putin.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako