• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marais wa China na Russia wapongezana kwa ushindi wa uchaguzi mkuu

  (GMT+08:00) 2018-03-20 09:23:21

  Rais Xi Jinping wa China na rais Vladimir Putin wa Russia jana waliwasiliana kwa njia ya simu na kupongezana kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu, pia wameahidi kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

  Rais Xi Jinping amesema kuendelea kwa Bw. Putin kuwa rais wa Russia ni chaguo sahihi la wananchi wa Russia, na anaamini kuwa warussia wanaweza kuendelea kupata mafanikio kwenye maendeleo na ustawi wa taifa.

  Rais Xi Jinping amesema anakubaliana na mapendekezo muhimu yaliyotolewa na rais Putin kuhusu ujenzi wa taifa, kuboresha maisha ya wananchi na kuhimiza uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia. Ameeleza imani yake kuwa China na Russia zikifuata njia zao za kujiendeleza, hakika zitapata mafanikio mapya katika siku zijazo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako