• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China asisitiza hakuna nguvu yoyote duniani inayoweza kuzuia watu wa China kutimiza ndoto yao

  (GMT+08:00) 2018-03-20 11:25:03

  Rais Xi Jinping wa China amesema ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya unahusisha kila mtu wa China, na kama wakishikamana na kufanya bidii kwa pamoja, hakuna nguvu yoyote duniani inayoweza kuwazuia watu wa China kutimiza ndoto yao.

  Rais Xi amesema hayo alipohutubia sherehe ya kufungwa kwa Mkutano wa kwanza wa awamu ya 13 ya Bunge la umma la China iliyofanyika leo asubuhi hapa Beijing, ikiwa ni mara ya kwanza kwa rais Xi kutoa hotuba baada ya kuchaguliwa kuwa rais kwa awamu nyingine.

  Pia amesisitiza kuwa ataendelea kutekeleza kwa makini na kikamilifu wajibu na majukumu aliyopewa na katiba ya nchi kama alivyofanya zamani, na kuendelea kuwahudumia wananchi na kusimamiwa na wananchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako