• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa China asema China daima haitafanya upanuzi

  (GMT+08:00) 2018-03-20 12:53:24

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo hapa Beijing amesema, China daima haitafanya upanuzi, na itafanya juhudi za kujihusisha na mambo yake yenyewe.

  Bw. Li Keqiang amesema, China inapenda kukuza uhusiano na nchi mbalimbali duniani kwa kufuata msingi wa kuheshimiana na kunufaishana, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma moja.

  Amesema China italinda ukamilifu wa ardhi, kamwe haitaacha sehemu yoyote ya ardhi, lakini haitakalia ardhi za nchi nyingine.

  Amesisitiza kuwa China inakabiliwa na matatizo na changamoto katika mchakato wa kujiendeleza, hali ambayo inahitaji mazingira ya amani na utulivu ya kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako