• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China na Afrika kujenga pamoja "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ili kuhimiza zaidi maendeleo ya ushirikiano kati yao

  (GMT+08:00) 2018-03-20 16:29:57

  Balozi wa wizara ya mambo ya nje ya China anayeshughulikia mambo ya Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC Bw. Zhou Yuxiao jana huko Nairobi amesema kuunganisha pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", ajenda ya mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika na mikakati ya kujiendeleza ya nchi mbalimbali za Afrika ili kuhimiza zaidi maendeleo ya ushirikiano kati ya China na Afrika, kutakuwa kauli mbinu ya mkutano wa kilele wa FOCAC utakaofanyika mwezi Septemba mwaka huu hapa Beijing.


  Bw. Zhou Yuxiao na wasomi wa taasisi za utafiti wa ushirikiano kati ya China na Afrika hivi karibuni wamefanya ziara nchini Ethiopia, Uganda na Kenya, na kufanya mawasiliano na maofisa na washauri mabingwa wa nchi hizo tatu kuhusu kauli mbiu na mambo makuu ya mkutano wa kilele wa FOCAC utakaofanyika Beijing. Bw. Zhou Yuxiao jana huko Nairobi alihojiwa na vyombo vya habari vya China na Kenya.

  Bw. Zhou Yuxiao alipozungumzia hali ya utekelezaji wa mipango 10 ya ushirikiano kati ya China na Afrika iliyotolewa kwenye mkutano wa kilele wa FOCAC uliofanyika mjini Johannesburg mwaka 2015, amesema "Kutokana na juhudi za pamoja za China na Afrika, mipango 10 iliyotolewa kwenye mkutano wa kilele wa Johannesburg yametekelezwa vizuri. Katika sekta ya ujenzi wa miundo mbinu, miradi mingi ya ujenzi wa reli, bandari na uwanja wa ndege imekamilishwa au inaendelea, na miradi mingine inayopangwa pia imepata maendeleo makubwa."


  Bw. Zhou Yuxiao amesema, kuunganisha pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", ajenda ya mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika na mikakati ya kujiendeleza ya nchi mbalimbali za Afrika ili kuhimiza zaidi maendeleo ya ushirikiano kati ya China na Afrika, kutakuwa kauli mbinu ya mkutano wa kilele wa FOCAC utakaofanyika mwezi Septemba mwaka huu.


  Anasema, "Tunaamua kufanya pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" liwe kauli mbiu ya mkutano wa kilele utakaofanyika baadaye mwaka huu, tunafikiria kuunganisha pendekezo hilo, ajenda ya mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika, ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa na mikakati ya kujiendeleza ya nchi mbalimbali za Afrika. China ina ndoto ya kutimizwa, nchi za Afrika pia zina ndoto zao za kutimizwa, na ndoto ya China na ndoto za Afrika zinaweza kuunganishwa. Tunaamini kupitia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya ushirikiano chini ya mfumo wa mkutano wa kilele wa FOCAC, ndoto za pande mbili zitatimizwa."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako