• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Faru mweupe mzee zaidi afariki nchini Kenya

  (GMT+08:00) 2018-03-20 19:34:57

  Faru pekee mweupe wa kiume aliyebaki duniani aina Northern White amefariki jana kwenye hifadhi ya Wanyamapori ya Ol Pajeta katika kaunti ya Laikipia, kaskazini mwa Kenya akiwa na umri wa miaka 45.

  Meneja mawasiliano wa hifadhi hiyo Elodie Sampere amesema, Faru huyo aitwaye Sudan amefariki kutokana na matatizo ya kiafya yanayotokana na umri, ambayo yalisababisha udhaifu kwenye misuli na mifupa yake, huku akiwa na vidonda vingi kwenye ngozi yake.

  Kifo cha Faru Sudan kimefanya idadi ya Faru weupe aina ya Northern White kubakia wawili tu wa kike, ambao bado wako kwenye hifadhi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako