• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu wa G20 wafunguliwa

  (GMT+08:00) 2018-03-20 19:40:06

  Mkutano wa mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu wa kundi la G20 umeanza jana huko Buenos Aires nchini Argentina.

  Wajumbe karibu 400 kutoka nchi 24 na mashirika 13 wakiwemo mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde, mkuu wa Benki ya Dunia Bw. Kim Yong, mkuu wa Benki Kuu ya Ulaya Bw. Mario Draghi na waziri wa fedha wa Argentina Bw. Nicolas Dujovne wamehudhuria mkutano huo.

  Ajenda zilizojadiliwa katika siku ya kwanza ya mkutano huo ni pamoja na changamoto zinazoukabili uchumi wa dunia, mustakabali wa kundi la G20 chini ya uvumbuzi wa sayansi na tekenolojia, na miundombinu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako