Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba muhimu katika Mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 la Umma la China, akionesha fahari kubwa juu ya ustaarabu wa China, upendo mkubwa kwa wananchi, imani thabiti kwa maendeleo ya China na matumaini ya kuwanufaisha binadamu. Hotuba hiyo imefuatiliwa na vyombo muhimu vya habari duniani, na kuzusha mjadala mkubwa kwenye jumuiya ya kimataifa.
Gazeti la Washington Post la Marekani limetoa ripoti ikisema, hotuba hiyo ya rais Xi imeonesha mafanikio ya kihistoria yaliyopatikana katika sekta mbalimbali nchini China, pia imesisitiza kuwa China itajenga mustakabali mzuri zaidi kwa njia ya kuimarisha na kuendeleza mfumo wa ujamaa wenye umaalumu wa China.
Shirika la habari la Uingerza Reuters limesema, hotuba ya Rais Xi imesisitiza matumaini ya kushirikiana na Taiwan katika kutumia kwa pamoja fursa nzuri za kujiendeleza, na kuhimiza mchakato wa kutimiza muungano kwa njia ya amani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |