• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa Afrika waahidi kuwajumuisha wakimbizi kwenye mifumo ya elimu

    (GMT+08:00) 2018-03-21 10:02:24

    Watunga sera na wataalamu wa Afrika wamesisitiza tena ahadi ya kuweka sera katika sekta ya elimu ambayo ni muhimu kwa mahitaji ya vijana waliopoteza makazi.

    Kwenye mkutano wa baraza la kikanda uliofanyika huko Nairobi, maofisa hao wamesema hatua ya upendeleo ilikuwa ni lazima kuhakikisha wahanga wa vita vya wenyewe kwa wenyewe au majanga ya asili wanaweza kupata elimu bora ili kurejesha maisha yao.

    Waziri wa elimu wa Kenya Bibi Amina Mohamed amesema upatikanaji wa elimu rasmi kati ya wakimbizi vijana, ni muhimu katika kuimarisha mchango wao katika kujenga upya nchi za Afrika zinazokumbwa na vita.

    Pia amesema kuna haja ya kuweka taratibu zenye ufanisi za kupunguza na kutatua athari zinazotokana na mgogoro katika utoaji elimu kwa vijana. Amesema mchango wa vijana katika kujenga upya nchi zao zilizokumbwa na mapambano, hauwezi kupuuzwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako