Sekta ya utalii nchini Kenya inaendelea kupata ushindani mkubwa kutoka vivutio vingine vya utalii katika soko la kimataifa kufuatia ukosefu wa mbinu za kisasa za kuvutia watalii.
Akiongea mjini Mombasa,Waziri Balala alitaja changamoto nyingine kama kutegemea utalii sehemu kadhaa nchini.
Alisema ipo haja kuwe na vivutio vipya vya utalii ili kuwavutia wageni nchini Kenya badala ya vile vya zamani hususan fuo za bahari na mbuga za wanyama.
Aidha Balala alisema ni lazima kukabiliana na changamoto zilizopo ili kuinua sekta hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |