• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wahimiza umuhimu wa kubadilishana taarifa za kijasusi ili kuzuia mashambulizi Somalia

    (GMT+08:00) 2018-03-22 09:24:21

    Maofisa wa ujasusi kutoka nchi zilizotumia vikosi kwenye tume ya umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM na wale wa Somalia, wamemaliza mkutano wao wa siku tatu mjini Mogadishu, na kutoa mwito wa kuchangia zaidi taarifa za kijasusi na habari, wakisema hatua hiyo ni muhimu katika kuzuia mashambulizi nchini Somalia.

    Akiongea kwenye ufungaji wa mkutano huo, mkurugenzi wa operesheni wa jeshi la Somalia Mohamed Sheikh Madobe ametoa mwito wa kuwepo kwa juhudi za pamoja kukusanya taarifa za kijasusi kwa ufanisi.

    Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo inasema, washiriki waliangalia vyanzo visivyo vya jadi vya habari, walijadili kuhimiza kupatiana taarifa za kijasusi, na matishio yanayoibuka kutoka kwa kundi la Al-Shabaab licha ya kuwa wapiganaji wa kundi hilo wamedhoofishwa kutokana na mashambulizi yanayofanywa na vikosi vya usalama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako