• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Facebook yakiri makosa ya kuibiwa kwa data za watumiaji

  (GMT+08:00) 2018-03-23 09:10:03

  Mkurungenzi mkuu mtendaji wa kampuni ya Facebook Bw. Mark Zuckerberg alipozungumzia tukio la kuibiwa kwa data za watumiaji alisema kampuni yake imefanya makosa katika kuhifadhi data za watumiaji, na ameahidi kuwa kampuni yake itachukua hatua kutatua tatizo hilo.

  Bw. Zuckerberg amesema kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba mtafiti wa Chuo Kikuu cha Cambridge amepata data za watumiaji wa Facebook na kuzipa kampuni ya uchambuzi wa data iitwayo Cambridge Analytica.

  Amesema Facebook ina wajibu wa kuhifadhi data za watumiaji, imefanya makosa, na inatakiwa kufanya kazi nyingi mapema.

  Hivi sasa tovuti nyingi zinaidhinisha hadhi ya watumiaji kwa akaunti za Facebook. Kampuni ya Facebook imetoa taarifa ikisema itachukua hatua kuzuia kampuni nyingine kupata data za watumiaji bila kuidhinishwa na Facebook.

  Hivi karibuni vyombo vingi vya habari vimesema data za watumiaji milioni 50 zimepatikana na kutumiwa na kampuni ya Cambridge Analytica, na kampuni ya Facebook ilitambua jambo hili, lakini haikutangaza kwa wakati.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako