• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kupunguzwa kwa riba kuleta mafanikio ya kiuchumi Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-03-23 17:48:42

    Mapendekezo yaliyotangazwa hivi majuzi na jumuiya ya mabenki Tanzania ya kushusha riba za mikopo kutoka asilimia 22 hadi asilimia 6 kwa benki za biashara nchini Tanzania yametajwa kuwa yataleta mafanikio kwa uchumi wa Tanzania.

    Azma hiyo ya kushusha riba ilitangazwa kwenye Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania uliofanyika mjini Dar es Salaam Jumatatu wiki hii chini ya uenyekiti wa Rais John Magufuli. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabenki Bw Charles Kimei amesema riba ya mikopo katika benki za biashara nchini humo imeshuka kwa asilimia 16 kutoka asilimia 22.

    Aidha Bw Kimei amefafanua kuwa jambo lililosababisha kuwepo kwa riba kubwa kwa wafanyabiashara kulitokana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutoza riba kubwa kwa benki zilizokuwa zikikopa kutoka kwao. Hata hivyo wataalamu wa uchumi wamesema faida sita zitakazopatikana kama mpango huo utatekelezwa ni kuwepo kwa ongezeko la mikopo, ongezeko la wakopaji, na ongezeko la biashara. Faida nyingi ni ongezeko la makusanyo ya kodi, ongezeko la ajira kwa wananchi masikini na ongezeko la miradi ya maendeleo katika sekta zote muhimu ikiwemo za elimu, afya na uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako