• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia Afrika kuongeza uwezo wake wa kulinda amani na usalama

  (GMT+08:00) 2018-03-23 19:50:03

  Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Ma Chaoxu ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuisaidia Afrika kuongeza uwezo wake wa kulinda amani na usalama.

  Akihutubia kwenye mkutano wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu tathmini ya suala la amani na usalama la Afrika, Bw. Ma amesema, China inasifu nchi za Afrika kwa kutatua masuala yao kwa njia ya kiafrika na kuongeza ujenzi wa mfumo wa kulinda usalama wa pamoja barani humo. Amesema jumuiya ya kimataifa inatakiwa kushikilia kiwango cha pamoja cha kupambana na ugaidi, kuunga mkono jitihada za Afrika katika jambo hilo, kusaidia Afrika kutatua vyanzo vya migogoro yake na kuheshimu haki ya nchi za Afrika katika kuongoza kutatua masuala ya usalama barani humo.

  Pia Bw. Ma amesema, kuongeza ushirikiano na nchi za Afrika ni kanuni ya kimsingi ya sera ya kidiplomasia ya China, na China itaendelea kutekeleza sera zenye nia thabiti na mtazamo sahihi wa kupata maslahi kwa Afrika na kuunga mkono zaidi maendeleo ya amani ya Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako