• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNICEF yatoa wito wa kuimarisha msaada wa kibinadamu kwa watoto wa Yemen

    (GMT+08:00) 2018-03-26 08:49:36

    Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema watoto zaidi ya milioni 11 nchini Yemen wanahitaji msaada wa kibinadamu, kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

    Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Mashariki ya kati na Kaskazini mwa Afrika Bw Geert Cappelaere amesema watoto watano wanauawa au kujeruhiwa kila siku nchini Yemen tangu hali ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ilipoanza kuwa mbaya mwezi Machi mwaka 2015.

    Takwimu zilizotolewa na UNICEF zinaonyesha zaidi ya nusu ya watoto nchini Yemen hawawezi kupata maji safi ya kunywa na hali nzuri ya afya ya umma, na watoto laki 4 wamekumbwa na upatiamlo mkali. Zaidi ya hayo, watoto takriban milioni 2 wameacha shule, laki 5 kati yao wamekumbwa na hali hiyo baada ya vita kupamba moto mwezi Machi mwaka 2015.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako