• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendelea kufungua sekta ya utoaji huduma

    (GMT+08:00) 2018-03-26 09:09:47

    Naibu waziri wa biashara wa China na naibu mwakilishi wa China kwenye mazungumzo ya biashara ya kimataifa Bw. Wang Shouwen, amesema China itafungua zaidi sekta ya utoaji wa huduma katika siku zijazo.

    Bw. Wang amesema kati ya sekta 160 za biashara ya huduma iliyowekwa na WTO, China imefungua sekta 120. Kwa hatua ijayo China itafungua sekta za fedha, mawasiliano ya simu, matibabu, elimu na matunzo ya uzeeni.

    Bw. Wang amesisitiza kuwa China siku zote inaunga mkono biashara huria na ya haki, itaweka mkazo katika ujenzi wa "Ukanda mmoja, Njia moja", na kuhimiza kufungua mlango kwa pande zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako