• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa watafuta kufanya mkutano wa mwisho kwa ajili ya kurekebisha makubaliano ya kisiasa ya Libya

    (GMT+08:00) 2018-03-26 09:16:42

    Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Bw. Ghassan Salame amesema atafanya jaribio la mwisho la kuitisha mkutano kati ya pande mbalimbali za Libya ili kurekebisha makubaliano ya kisiasa yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

    Bw. Salame amesema amesisitiza kwa spika wa baraza la chini la bunge la Libya mashariki mwa nchi Agila Saleh mahitaji ya kufanya uchaguzi kabla ya mwisho wa mwaka huu.

    Bw. Salame aliyasema hayo baada ya kukutana na Bw. Saleh mjini Al-Qubbah ambapo walijadili maendeleo mapya ya kisiasa nchini Libya na maandalizi ya uchaguzi ujao.

    Marekebisho ya makubaliano ya kisiasa ya Libya ni sehemu ya mpango uliotolewa na Bw. Salame mwezi Septemba mwaka jana kwa lengo la kukomesha mgogoro wa kisiasa wa Libya, ambao pia unahusu kufanya uchaguzi wa wabunge na rais kabla ya mwisho wa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako