• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaikumbusha Marekani kuhusu kanuni na sio nguvu kwenye biashara ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2018-03-27 09:16:43

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying ameikumbusha Marekani kuwa inatakiwa kujua kuwa kwenye karne ya 21 biashara inaongozwa na kanuni na sio mabavu.

    Bibi Hua amesema hayo kufuatia kauli iliyotolewa na makamu wa rais wa Marekani Bw Mike Pence aliyesema hatua inazochukua Marekani kwa sasa zina maana 'zama ya kusalimu amri kiuchumi imepita".

    Bibi Hua amesema China mara zote inafuata kanuni za Shirika la biashara duniani WTO na kufuata mfumo wa biashara ya pande nyingi kwa mujibu wa kanuni za WTO. Pia imekuwa inasisitiza uwepo wa kuheshimiana, usawa na kunufaishana, na kutatua mikwaruzano ya kibiashara kwa njia ya majadiliano.

    Wiki iliyopita Rais Donald Trump wa Marekani alisaini agizo la kutoza ushuru wa dola bilioni 60 za kimarekani kwa bidhaa kutoka China na kuweka vizuizi dhidi ya uwekezaji wa China nchini Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako