• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka la Ufukweni: CAF na FUFA wazindua ujenzi wa uwanja kwa ajili ya mashindano mjini Entebbe 

    (GMT+08:00) 2018-03-27 09:53:38
    Shirikisho la mpira wa miguu la nchini Uganda FUFA kwa kushirikiana na shirikisho la vyama vya soka barani Afrika CAF, jana limezindua rasmi mradi wa ujenzi wa uwanja wa soka la ufukweni (beach soccer) mjini Entebbe.

    Mradi huo ambao umegawanyika katika hatua tatu, ujenzi wa sehemu ya kuchezea, ujezi wa majukwaa na ofisi ndogo pamoja na ujenzi wa sehemu za biashara na burudani ndogo kuzunguka eneo hilo, unakadiriwa kuwa utakamilika mwezi mei.

    Kwa mujibu wa katibu mkuu wa CAF Amry Fahmy, ambaye alishiriki uzinduzi huo, amesema shirikisho lake limeamua kushirikiana Uganda kukamilisha mradi huo unaokadiriwa kugharimu dola za kimarekani laki mbili sawa na shilingi za Uganda milioni 720, kwa kuwa Uganda wamechaguliwa kuwa wenyeji wa mashindano ya Afrika ya mwezi Mei.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako