• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa zaidi ya elfu 9 nchini China waadhibiwa kwa kukiuka kanuni cha Chama katika miezi miwili ya mwanzo ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-03-27 16:37:07

    Jumla ya maofisa 9,231 wameadhibiwa kwa kukiuka kanuni za Chama cha Kikomunisti cha China katika miezi miwili ya mwanzo ya mwaka huu.

    Taarifa iliyotolewa kwenye tovuti ya Kamati ya Ukaguzi wa Nidhamu ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imesema, idadi hiyo ilikusanywa kutoka mikoa 31, idara 139 za Chama na serikali, kampuni 97 zinazomilikiwa na serikali, taasisi 15 za kifedha zinazosimamiwa na serikali kuu, pamoja na kundi la wanajeshi wanaoshughulikia uzalishaji na ujenzi mkoani Xinjiang.

    Mwaka 2012, CPC ilipitisha kanuni nane za utendaji wa Chama na serikali kwa lengo la kuboresha utendaji kazi. Mwaka jana, zaidi ya maofisa elfu 71 waliadhibiwa kwa makosa ya kukiuka kanuni hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako