• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Israel lakamata wenyeji watatu wa Gaza walioingia Israel wakiwa na visu na maguruneti

    (GMT+08:00) 2018-03-28 09:03:46

    Jeshi la Israel limewakamata watu watatu kutoka ukanda wa Gaza walioingia kiharamu nchini Israel, wakiwa na visu na maguruneti. Jeshi hilo limesema watuhumiwa hao walivuka uzio wa usalama ulioko kusini mwa Gaza, na kusafiri umbali wa kilomita 20 kwenye ardhi ya Israel, kabla ya kukamatwa na wanausalama. Hii ni mara ya pili kwa watu wa Gaza kuingia kiharamu nchini Israel ndani ya wiki hii. Taarifa iliyotolewa na polisi nchini Israel inasema hivi sasa watuhumiwa hao wanahojiwa na wameimarisha hatua za usalama kwenye eneo la tukio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako