• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Michezo ya Jumuiya ya Madola: Rais Kenyatta aagiza wanamichezo wote wanaokwenda Australia wote wawe wamelipwa stahili zao zote itakapofika saa saba mchana leo

  (GMT+08:00) 2018-03-28 10:44:58

  Rais Uhuru Kenyatta amemwagiza waziri wa michezo Rashid Echesa kuhakikisha zoezi la kuwalipa stahili zao zote wanamichezo wa Kenya wanaokwenda kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola nchini Australia linakamilika mapema leo kabla ya saa saba mchana kwa saa za Afrika Mashariki.

  Pia Rais Kenyatta ameiagiza wizara ya michezo kufanya mapitio, ili kubaini madai na malimbikizo ya malipo ya michezo na stahili za wanamichezo nchi nzima ya tangu mwaka 2002, na kuhakikisha yote yanalipwa.

  Akizungumza na wanamichezo wanaokwenda Australia, Rais amewapongeza kutokana na juhudi zao kubwa na amewataka kuendeleza moyo wa uzalendo kuipigania nchi yao kwa nguvu kupitia michezo, akisema serikali itatimiza wajibu wake kuwatunza tangu mwanzo hadi mwisho wa mashindano.

  Lakini pia ametumia mkutano huo na wanamichezo hao, kuwakumbusha viongozi wa vyama vyote vya kimichezo kutimiza wajibu wao ili taifa liendelee kukua katika viwango vya dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako