• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ina nia ya kuisaidia Afghanistan kutimiza mapema amani na maendeleo

    (GMT+08:00) 2018-03-28 17:24:08

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Li Baodong amesema, China iko tayari kuhimiza ushirikiano wa nyanja mbalimbali na Afghanistan na kuisaidia kutimiza mapema amani na maendeleo.

    Bw. Li amesema hayo kwenya mkutano wa ngazi ya juu kuhusu suala la Afghanistan uliofanyika Tashkent, mji mkuu wa Uzbekistan. Kauli mbiu ya mkutano huo ni "mchakato wa amani, ushirikiano wa usalama na mawasiliano ya kikanda".

    Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe zaidi ya 20 kutoka Afghanistan, Pakistan, Iran, Marekani, Russia, China, pamoja na Umoja wa Mataifa, na Umoja wa Ulaya. Wajumbe hao wamejadili masuala ya mchakato wa maelewano nchini Afghanistan, kukabiliana na tishio la ugaidi kwa pamoja, kukuza ushirikiano wa uchumi na mawasiliano ya kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako