• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jopo la washauri bingwa wa China latoa mapendekezo ya kukabliana na hali ya wasiwasi ya biashara kati ya China na Marekani

    (GMT+08:00) 2018-03-28 17:35:01
     

    Kituo cha washauri bingwa cha China na Utandawazi CCG kimetoa mapendekezo kumi ya kukabiliana na hali ya wasiwasi ya biashara na kudumisha utulivu kati ya China na Marekani

    Mapendekezo hayo ni pamoja na kujadili kuanzisha mfuko wa uwekezaji wa miundombinu kati ya China na Marekani na kuhimiza kufikiwa kwa makubaliano ya biashara ya kielektroniki kati ya nchi hizo mbili. Kituo hicho kimependeza kuwa China inatakiwa kuongeza ufahamu wa raia wa Marekani kuhusu hali halisi ya pengo la biashara kati ya nchi hizo mbili katika mazingira ya utandawazi wa dunia, kuongeza bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani, kupunguza ushuru wa bidhaa za magari, simu za mkononi na bidhaa za kifahari, kuagiza zaidi bidhaa za nishati na mazao za Marekani nchini China.

    Kituo hicho pia kimeipendekeza China kufungua mlango zaidi, kuweka mazingira yanayosaidia maendeleo ya uwekezaji kutoka nje, na kuzifanya kampuni za nchi za nje zihimize serikali zao kuacha msimamo wao wa kujilinda kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako