• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa ataka kuwepo kwa hatua za pamoja kukabiliana na changamoto za ulinzi wa amani

    (GMT+08:00) 2018-03-29 09:05:41

    Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa mwito wa kuwepo kwa hatua za pamoja zenye nguvu ili kukabiliana na changamoto kubwa za ulinzi wa amani za umoja wa mataifa.

    Amesema shughuli za ulinzi wa amani za umoja wa mataifa kwenye nchi zenye walinzi wengi zaidi wa amani yaani Mali, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya kati na Sudan kusini zinakabiliwa na changamoto kubwa. Amesema kwa sasa shughuli za ulinzi wa amani za umoja wa mataifa zinafanyika katika mazingira magumu, tata na yenye hatari. Amesema mwaka jana walinzi 59 wa amani waliuawa, likiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na walinzi 34 wa mwaka 2016.

    Mjumbe wa China kwenye Umoja wa mataifa Bw Ma Zhaoxu, amesema shughuli za ulinzi wa amani zinatakiwa kufuata katiba ya umoja wa mataifa na kuheshimu uhuru wa nchi zinazowapokea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako