• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iraq yasema haitaki kujiingiza kwenye mgogoro kati ya Marekani na Iran

    (GMT+08:00) 2018-03-29 09:09:20

    Waziri mkuu wa Iraq Bw. Haider al-Abadi amesema Iraq haitaki kujiingiza kwenye mgogoro kati ya Marekani na Iran. Akihutubia mkutano wa Baraza la nishati la Iraq uliofanyika jana mjini Baghdad, Bw. Al-Abadi amesema Iraq inataka kudumisha uwiano wakati wa kushughulikia uhusiano kati yake na Iran na Marekani, na kwamba kutojiingiza kwenye mgogoro kati ya Iran na Marekani kunalingana na maslahi ya Iraq. Bw. Al-Abadi pia ametoa mwito kwa Marekani kutojitoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya Iran yaliyofikiwa mwaka 2015.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako