• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya kimataifa yafuatilia ziara ya Bw. Kim Jong-un nchini China

    (GMT+08:00) 2018-03-29 10:03:43

    Kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong-un amefanya ziara isiyo rasmi nchini China kuanzia tarehe 25 hadi 28 Machi kutokana na mwaliko wa rais Xi Jinping. Jumuiya ya kimataifa inaona kuwa ziara hiyo ina umuhimu mkubwa katika kupunguza zaidi mvutano katika Peninsula ya Korea.

    Wizara ya mambo ya nje ya Russia imetoa taarifa ikisisitiza kuwa inapenda kuendelea kushirikiana kwa karibu na upande wa China, katika kuhimiza mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande husika, ili suala la peninsula ya Korea litatuliwe kwa njia ya kisiasa na kidiplomasia.

    Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kusini imetoa maelezo ikisema Korea Kusini inatumai kuwa ziara ya kiongozi wa Korea Kaskazini nchini China itasaidia kutimiza lengo la kuondoa silaha za nyuklia kwenye Peninsula ya Korea, na kujenga amani katika eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako