• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Miundombinu hafifu yakwamisha jitihada za miji ya Afrika kutumia TEHAMA

    (GMT+08:00) 2018-03-29 10:04:14

    Wataalamu wa maendeleo ya miji na teknolojia wamesema miundombinu hafifu ni changamoto kubwa kwa miji ya nchi za Afrika kujiendeleza kiuchumi kuelekea kueneza matumizi ya TEHAMA.

    Wataalamu wamesema hayo katika Mkutano wa mwaka 2018 wa Baraza la Kimataifa la Next Einstein NEF unaofanyika mjini Kigali, Rwanda.

    Msaidizi wa profesa wa mtandao wa dunia katika Chuo Kikuu cha New York cha Marekani Bw. Hamidou Tembine, amesema miundombinu hafifu barani Afrika kama vile mtandao wa barabara na reli, nishati na upashanaji wa habari imekwamisha ukuaji wa uchumi, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mipango ya kuendeleza miji inayotumia TEHAMA.

    Upungufu wa miundombinu ya TEHAMA barani Afrika ni fursa kwa wanasayansi wa Afrika kuunda mifumo ya kisasa zaidi ili kukabiliana na changamoto kwa miji barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako