• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpira wa Wavu: Timu ya GSU ya Kenya yashinda mechi mbili mfululizo katika mashindano ya ubingwa wa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-03-29 10:30:01

    Timu ya mpira wa Wavu ya GSU kutoka Kenya jana imepata ushindi wa seti 3-1 katika mechi yake ya pili dhidi ya Wolaitta ya Ethiopia kwenye masindano ya klabu bingwa Afrika yanayoendelea nchini Misri.

    Huu ni ushindi wa pili mfululizo baada ya kuifunga timu ya Olympique kutoka Algeria kwenye mechi ya kwanza, na timu hiyo iliyoko kundi D la Mashindano leo inacheza na timu ya Port kutoka Cameroun.

    Endapo GSU itashinda mechi dhidi ya Port, moja kwa moja itafuzu hatua ya mtoano ya mashindano hayo.

    GSU ambao ni mabingwa wa Kenya kwenye ligi ya mchezo wa mpira wa wavu wamerejea kwa kasi katika mashindano ya Afrika baada ya kukosekana msimu uliopita nchini Tunisia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako