• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michezo ya Afrika Mashariki: Rwanda yaendelea na maandalizi kwa ajili ya mashindano ya shule za sekondari

    (GMT+08:00) 2018-03-29 10:30:53

    Serikali ya Rwanda imeendelea kuuandaa mji wa Musanze ulioko kaskazini mwa nchi hiyo kwa kuwa ndiyo utakuwa kitovu cha mashindano ya michezo kwa shule za sekondari kutoka nchi za Afrika Mashariki 'FEASSSA' mwezi Agosti mwaka huu.

    Kwa mujibu wa Mkuu wa FEASSSA ambaye ni kiongozi wa walimu wa michezo katika mji wa Musanze, Jean Twagirimana maandalizi hayo pamoja na mambo mengine yamehusisha ukarabati wa viwanja saba vya mpira wa miguu, ambapo vitatu kati ya hivyo vimekarabatiwa kulingana na ushauri wa kitaalamu ili kukidhi mahitaji.

    Takribani wanamichezo 4,000 watashiriki matukio tofauti ya kimichezo, na wote hao ni kutoka nchi 6 za Afrika Mashariki ambazo ni Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Tanzania na Sudan Kusini.

    Hii ni mara ya pili kwa Rwanda kuandaa mashindano hayo baada ya kufanya hivyo pia mwaka 2015.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako