• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kriketi: Wachezaji watatu wa Australia wafungiwa kutokana na udanganyifu

    (GMT+08:00) 2018-03-29 10:31:50

    Wachezaji watatu wa Kriketi kutoka timu ya taifa ya Australia Steve Smith, Cameroun Bancroft na nahodha msaidizi wa timu hiyo David Warner wamefungiwa kutojihusisha na mchezo huo ndani na nje ya nchi hiyo kutokana na udanganyifu waliofanya ili kupata matokeo chanya.

    Smith na Warner wamefungiwa kutoshiriki kwa kipindi cha miezi 12, lakini Cameroun ambaye anahusishwa na kashfa ya kufanya uhujumu kwenye mechi mojawapo kwa kuharibu kwa makusudi mpira amefungiwa kwa miezi tisa.

    Vifungo hivyo vilivyotolewa kwa mujibu wa kanuni za baraza la mchezo wa Kriketi duniani ICC, vinawazuia wachezaji hao kutoshiriki hata katika michezo ya ligi za ngazi ya klabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako