• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni ya China AVIC International yafanya juhudi kuwapa vijana mafunzo ya kiufundi nchini Kenya

  (GMT+08:00) 2018-03-29 18:03:02

  Serikali ya Kenya imeipongeza kampuni ya Kichina ya AVIC International kwa juhudi zake za kuwapa vijana mafunzo ya kiufundi nchini Kenya. AVIC International kupitia mradi wa Africa TYech Challenge, imekuwa ikiwapa vijana nchini Kenya mafunzo ya useremala, kutengeneza matofali, ujenzi miongoni mwa mafunzo mengine. Akiongea wakati wa hafla ya kuwatuza vyeti vijana waliohitimu na AVIC International, mgeni wa heshima ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Bi Amina Mohammed, aliisifia sana kampuni za Kichina kwa kuendelea kutoa mafunzo ya kiufundi kwa vijana nchini humo.

  Ulikuwa usiku wa kipekee kwa vijana zaidi ya ishirini waliokuwa wakituzwa vyeti kwa kuhitimisha mafunzo yao na kampuni ya kichina ya AVIC. Kupitia kitengo chake cha Africa Tech Challenge yaani ATC, makumi ya vijana chini ya mradi wa Jenga Vijana, ilitoa fursa ya kipekee kwa vijana hawa kupewa mafunzo mengi ya kiufundi, ambayo sasa wako tayari kunufaika nayo.

  Naitwa Alexander Mogele. Nimekuja ATC, nikafunzwa kuhusu useremala. Sikuwa najua chochote ila sasa najua mengi.

  Jina langu ni Margeret Wambui. Mimi ni mjenzi.

  Naibu Rais wa kampuni ya AVIC International bwana Liu Jun aliwapongeza vijana hawa na kuahidi kuwa huu ndio mwanzo tu wa kuwasaidia vijana hapa nchini Kenya.

  'Kampuni ya kimataifa ya AVIC, inaamini kuwa ni lazima tuwawezeshe vijana wetu katika kila sekta maishani. Hii itawapa fursa nzuri ya kutengeneza nafasi za ajira na hata kuwapa maarifa yanayohitajika na waajiri wengine. Ni kutokana na sababu kama hizi ndiposa Africa TECH Challenhe ikazinduliwa. Tunafurahia matunda yetu na ushirikiako uliopo kati yetu na nyinyi tunaofanya kazi pamoja. Tuna kibarua cha ziada kuhakikisha kuwa tunapunguza idadi ya vijana wasio kuwa na ajira nchini.'

  Akizungumza kwenye hafla hiyo, Balozi wa China nchini Kenya Liu Xianfa alisema kwamba kuna takribana kampuni 400 za Kichina nchini Kenya na zinapaswa kuiga mfano wa AVIC kwa kutoa mafunzo kwa wafanyikazi wake ili kuwafaa zaidi.

  'Ni kutokana na sababu hii ndiposa serikali ya China kupitia ubalozi wake hapa nchini imetoa udhamini wa masomo na vile vile nafasi kwa vijana kujifunza maswala ya ufundi mbali mbali. Mwaka wa 2017, tulitoa udhamini wa masomo kwa vijana 230 na zaidi ya nafasi 700 za mafunzo kwa vijana wa taaluma mbalimbali. Tunahimiza kampuni za Kichina zilizopo hapa nchini kuiga mfano huu wa kuwapa udhamini na mafunzo wafanyikazi wao wa hapa nchini.'

  Mgeni wa heshima ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Satyansi na Teknolojia nchini Kneya Bi Amina Mohammed, aliahidi kuwa Wizara yake itatoa mazingira mwafaka ya kukuza na kuwasaidia vijana ili kuendeleza ustawi wa taifa.

  'Mabibi na mabwana, ufanisi huu ambao tunaushuhudia hapa, umesaidia wizara ya Elimu katika kurahisisha na kuimarisha malengo yake ya Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi. Ningependa kuwahakikishia ushirikiano thabiti kutoka kwa wizara yangu, ili kuhakikisha kuwa tunatoa nafasi zaidi za kuwapa vijana wetu mafunzo ili kuimarisha ukuaji wa viwanda wa taifa letu tukufu.'

  Kwa vijana hawa, hawangeficha furaha yao kwani baadhi yao tayari wamepewa ajira na kampuni ya AVIC kupitia Africa Tech Challenge ATC.

  Naitwa Peter Muremi Njoki. Nimefunzwa useremala. Hii challenge imenisaidia sana. Nimefunzwa hadi nikapa kazi.

  Penye nia, siku zote pana njia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako