• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wapitisha msimamo wa pamoja wa nafasi ya Afrika katika uhusiano wake na Umoja wa Ulaya baada ya mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2018-03-29 19:18:10

    Kamati ya Utendaji ya Umoja wa Afrika imepitisha msimamo wa pamoja wa Afrika kwa ajili ya majadiliano ya makubaliano mapya ya ushirikiano na Umoja wa Ulaya.

    Uamuzi wa kuwa na msimamo wa pamoja ulifikiwa wiki iliyopita katika tukio la kihistoria barani Afrika, ambapo nchi wanachama 44 wa Umoja wa Afrika walisaini mpango wa kuanzisha Eneo la Biashara Huria la Afrika, ambalo Umoja huo unasema kuwa ni sauti kubwa na ya nguvu kwa dunia kuwa Afrika inaweza kuungana na kuongea kwa sauti moja.

    Nchi zinazoendelea za Afrika, Caribbean na Pasific zilisaini makubaliano ya uhusiano na Umoja wa Ulaya, mjini Cotonou, Benin, mwaka 2000 kwa kipindi cha miaka 20 mpaka mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako