• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Namibia wakutana Beijing

    (GMT+08:00) 2018-03-30 08:34:33

    Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na mwenzake wa Namibia Bw. Hage Geingob, ambaye ni mgeni wa pili kwa rais Xi kutoka Afrika katika wiki moja iliyopita.

    Rais Xi amesema China na Afrika ziko katika jumuiya yenye hatma ya pamoja, na zina maslahi ya pamoja yanayonufaisha pande zote. China itaendelea kuzisaidia nchi za Afrika kuongeza uwezo wa kupata maendeleo endelevu kwa kujitegemea. Anaamini kuwa China na Afrika zitashirikiana kuanzisha Jumuiya ya hatma ya pamoja, na kuongeza msukumo mpya kwa ajili ya maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili.

    "Hivi sasa China inadhamiria kujenga nchi ya kisasa ya ujamaa wenye umaalumu wa China kwa kufuata malengo mapya yaliyothibitishwa kwenye Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha kikomunisti cha China, wakati Namibia inaharakisha mchakato wa maendeleo ya viwanda na mambo ya kisasa, ili kutimiza lengo la kujitegemea kiuchumi na kutokomeza umaskini. China inapenda kushirikiana na Namibia kuimarisha ushirikiano, ili kuwanufaisha watu wa pande zote mbili."

    Kwa upande wake rais Geingob anasema,

    "Namibia inaweka mkazo katika kukuza uhusiano na China. Hivi sasa tunapaswa kuimarisha ushirikiano katika sekta za miundombinu, raslimali watu, utamaduni na elimu. Ushirikiano katika sekta hizo umeonesha umuhimu wa mawasiliano kati ya pande hizo mbili."

    Viongozi hao wamekubaliana kuanzisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote. Rais Xi amesema China inakaribisha Namibia kujiunga na ujenzi wa "Ukanda mmoja, Njia moja", pia inapenda kushirikiana na Namibia kutumia fursa kwa pamoja, kuimarisha mawasiliano ya kisera na uratibu wa mipango, ili kusukuma mbele ushirikiano katika sekta muhimu.

    Baada ya mazungumzo hayo, viongozi hao wameshuhudia kwa pamoja kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano katika sekta za miundo mbinu, fedha na afya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako