• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yazindua tovuti ya habari za kibiashara kuhimiza maendeleo ya biashara

    (GMT+08:00) 2018-03-30 09:44:11

    Idara ya mapato ya Rwanda RRA imezindua tovuti ya huduma kwenye mtandao ambayo habari zote kuhusu uuzaji nje, uingizaji na usafirishaji wa bidhaa zitapatikana bure kwa mashirika ya kibiashara, idara za serikali na pande zote husika.

    Idara hiyo imesema tovuti hiyo inaweza kusaidia wafanyabiashara kuharakisha mchakato wa kibiashara, na kuongeza kasi ya mchakato wa kuagiza kwa asilimia 47 na kuuza bidhaa nje kwa asilimia 91.

    Waziri wa biashara wa viwanda Bw. Vincent Munyeshyaka amesema, tovuti hiyo itaboresha mazingira ya kufanya biashara nchini humo kwa kupunguza muda na gharama za kutafuta habari husika na kuongeza ufanisi wa kufanya biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako