• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Zambia yaahidi kulipa mishahara iliyocheleweshwa ya wafanyakazi wa TAZARA

    (GMT+08:00) 2018-03-30 09:44:31

    Serikali ya Zambia imeamua kulipa mishahara iliyocheleweshwa ya wafanyakazi wa TAZARA baada ya wafanyakazi kutishia kugoma.

    Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyakazi ya TAZARA Bw. Bedwin Malowa, amesema wafanyakazi hawawezi kuvumilia zaidi serikali kuendelea kushindwa kulipa mishahara yao kwa miezi mitatu, hasa baada ya kufanya mazungumzo mengi na idara husika.

    Lakini kwa upande wake, waziri wa uchukuzi na mawasiliano wa Zambia, Brian Mushimba amesema, kutokana na kuharibika kwa miundo mbinu, TAZARA haiwezi kupata mapato ya kutosha kulipa mishahara. Hivi sasa, serikali imepata fedha za kutatua suala hilo na kuwataka wafanyakazi hao wasigome.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako