• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kufanyika uchunguzi juu ya mgogoro uliozuka Gaza

    (GMT+08:00) 2018-03-31 18:20:04

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi huru na wa uwazi kuhusu mapigano makali kati ya vikosi vya usalama vya Israel na waandamaji wa kipalestina mjini Gaza.

    Katibu huyo amewataka wote wanaohusika kuachana na vitendo kama hivyo ambavyo amedai vinaweza kusababisha kuongezeka kwa vifo ama vinaweza kuwaumiza kwa njia yoyote raia waeneo hilo.

    Taarifa ya wito huo wa katibu mkuu inakuja baada ya wapalestina wasiopungua 15 kuuawa na wanajeshi wa Israel kwenye uzio wa mpaka wa Gaza na wengine mamia wakiripotiwa kujeruhiwa.

    Kutokana na tukio hilo, katibu mkuu Guterres amesema ipo haja ya kuharakisha uanzishwaji upya wa mchakato wa amani yanayolenga kuandaa mazingira bora ya mazungumzo kwa ajili ya suluhu itakayowapa fursa waPalestina na waisreal kuishi kwa amani na usalama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako