• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tangazo la Trump la kuyaondoa majeshi ya Marekani nchini Syria katika siku za hivi karibuni lazua utata

    (GMT+08:00) 2018-03-31 18:20:32

    Rais Donald Trump amesema serikali ya Marekani itayaondoa majeshi yake yaliyoko Syria katika siku za hivi karibuni.

    Taarifa hiyo iliyotolewa na Ikulu ya Marekani imezusha maswali mengi kwa maafisa wa jeshi la Marekani ambao walidai kutokuwa na taarifa juu ya uamuzi huo.

    Siku ya Alhamis, Trump alisikika akisema hivi karibuni watayaondoa majeshi Syria ili kutoa nafasi kwa watu wengine kushughulikia suala la Syria.

    Trump aliongeza kuwa, kwa kuwa wameamua kuachana na ISIS, hivyo wataondoka katika siku za hivi karibuni, ili kurudi nchini Marekani ambako amedai ndiko wanakohitaji zaidi.

    Kauli hiyo ya Trump imeelezwa kuleta mkanganyiko kwenye msimamo wa Jeshi la Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako