• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vurugu katika eneo la Gaza zazuka tena, na watu 35 wamejeruhiwa

    (GMT+08:00) 2018-04-01 19:14:21

    Wapalestina 35 wamejeruhiwa baada vurugu zilizozuka tena jana mchana kati ya waandamanaji wa kipalestina na wanajeshi wa Israel.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na msemaji wa wizara ya afya katika eneo la Gaza, Ashraf al Qedra, majeruhi hao ambao ni vijana wa kipalestina, waliumia baada ya majeshi ya Israel kushawambulia kwa risasi, na wote wamefikishwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

    Kuhusu hali za majeruhi hao, al Qedra amesema wengi wao wapo katika hali isiyokuwa hatari, na baadhi yao walinusurika kufuatia madaktari wa Palestina kuwatibu baada ya kupigwa mabomu ya machozi.

    Ni siku ya pili ambapo vurugu zimetokea katika eneo la Ukanda wa Gaza kati ya mamia ya waandamanaji na wanajeshi wa Isreal karibu na uzio wa mpaka baina ya Palestina na Israel.

    Awali bwana Al Qedra alisema Siku ya Ijumaa wapalestina 15 waliuawa na wengine 1,416 walijeruhiwa kutokana na vurugu hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako