• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Masisi aapishwa kuwa rais mpya wa Botswana

    (GMT+08:00) 2018-04-02 08:51:31

    Bw. Mokgweetsi Masisi jana aliapishwa na kuwa rais mpya wa Botswana huko Gaborone, mji mkuu wa nchi hiyo.

    Masisi ni rais wa awamu ya tano katika historia ya nchi hiyo, na anachukua madaraka kutoka kwa rais wa zamani Bw. Seretse Khama Ian ambaye alimaliza muda wake wa mihula miwili tarehe 31 mwezi Machi.

    Rais Masisi amesema kuna haja ya kujenga Botswana yenye maendeleo endelevu kwa msingi wa kuwa na uchumi unaoshirikisha pande mbalimbali.

    Rais Masisi pia amesisitiza kuwa atafanya juhudi kupunguza utegemezi wa uchumi kwenye almasi, kuongeza nafasi za ajira kwa mtu mmoja kati ya watano wasiokuwa na ajira, na kuvutia uwekezaji zaidi kutoka nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako