• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Anthony Joshua ajibu kwa kusema yuko tayari kupigana nje ya Uingereza

    (GMT+08:00) 2018-04-02 10:00:51

    Baada ya mwingereza Anthony Joshua AJ kushinda na kutwaa taji kubwa la ubingwa wa masumbwi la WBO wikendi hii alipomtwanga Joseph Parker, wachambuzi wachambuzi wa mchezo huo wameanza rasmi kusubiri tangazo la kuanza kwa mchakato wa safari yake ya kuwania mkanda mwingine wa WBC unaoshikiliwa na Wilder Deontay wa Marekani.

    Wilder amekaririwa akisema Joshua anapata ushindi kutokana na upendeleo na hata hivyo hajawahi kushinda akiwa nje ya Uingereza, sasa amewataka mapromota kuzingatia hilo.

    Kwa upande wake AJ ametangaza kuwa hana tatizo na jambo hilo na yuko tayari kutoka na kwenda kupigana nje ya Uingereza na hasa kuwania huo mkanda wa WBC.

    Joshua mwenye miaka 28, ni bingwa wa uzito wa juu mwenye mikanda mitatu ya WBO, IBF na WBA na hajawahi kupoteza hata pambano moja kati ya 21 aliyowahi kupigana na 20 ikiwa ni kwa Knock-Out.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako