• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais mpya wa shirikisho la mpira wa miguu asema atawekeza zaidi kuendeleza soka la vijana

    (GMT+08:00) 2018-04-02 10:03:08

    Rais mpya wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Rwanda FERWAFA, Jean-Damascène Sekamana amesema moja ya malengo aliyojiwekea ili kuendeleza kiwango cha mchezo huo ni kuhimiza umoja wa watendaji na wadau wote wa mchezo huo, na kubwa zaidi atahakikisha anaendeleza soka la vijana kwa kuibua vipaji na kuvitunza.

    Sekamana alitoa kauli hizo baada ya kuibuka mshindi kwenye uchaguzi uliofanyika jana ambapo alipata kura nyingi kuliko mpinzani wake kwenye kinyang'anyiro hicho Louis Rurangirwa sasa anachukua nafasi inayoachwa wazi na Vincent Nzamitwa.

    Sekamana ambaye ni Rais wa zamani wa klabu ya Kiyovu anatarajiwa kuongoza FERWAFA kwa miaka minne ikiwa ni kipindi cha kwanza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako