• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ujenzi wa Xiong'an kutoa uzoefu kwa maendeleo ya kikanda nchini China

  (GMT+08:00) 2018-04-02 17:37:33

  Tarehe mosi Aprili ni mwaka mmoja tangu China ianze kujenga eneo jipya la Xiong'an. Wataalamu walipohojiwa na waandishi wetu wa habari wamesema, katika mwaka mmoja uliopita, China imeshikilia "mtizamo na vigezo vya kimataifa, umaalumu wa China na ngazi ya juu" katika ujenzi wa eneo hilo, mji wa Xiong'an utatoa uzoefu katika uhifadhi wa mazingira, teknolojia za hali ya juu za kidijitali na uvumbuzi kwa ajili ya maendeleo ya sehemu za Beijing, Tianjin na Hebei, na maendeleo ya kikanda katika sehemu nyingine nchini China.

  Katika mwaka mmoja uliopita, mchakato wa kujenga eneo jipya la Xiong'an umepiga hatua kubwa katika ujenzi wa miundo mbinu na ajira. Mkuu wa taasisi ya utafiti wa mageuzi na maendeleo ya mkoa wa Hainan, China Bw. Chi Fulin amesema, ujenzi wa eneo hilo umefanya maendeleo ya ushirikiano kati ya sehemu za Beijing, Tianjin na Hebei yapige hatua mpya. Anasema,

  "Ujenzi wa eneo jipya la Xiong'an umefanya maendeleo ya ushirikiano kati ya sehemu za Beijing, Tianjin na Hebei yapige hatua mpya. Nafikiri mwaka huu, kutokana na ujenzi wa eneo hilo, maendeleo ya ushirikiano kati ya sehemu za Beijing, Tianjin na Hebei yatafungua ukurasa mpya."

  Kwa mujibu wa mpango uliowekwa, eneo jipya la Xiong'an litapokea shughuli zisizohusika na mji mkuu za Beijing, haswa shughuli za sayansi na teknolojia. Hadi sasa makampuni zaidi ya mia moja ya sayansi na teknolojia za ngazi ya juu yameanzisha shughuli katika eneo hilo. Naibu mkuu wa taasisi ya sayansi za miji na sehemu ya Chuo Kikuu cha Fedha cha Shanghai Bw. Zhang Xueliang anasema,

  "Katika mwaka mmoja uliopita tangu kuanzishwa kwa eneo jipya la Xiong'an, China imefanya majaribio ya kuhamisha shughuli zisizo za mji mkuu, za Beijing na kupeleka eneo la Xiong'an. Nimeona makampuni mengi ya Beijing na miji na mikoa mingine yameanzisha shughuli katika eneo hilo. Naona eneo hilo litatoa mchango kwa maendeleo ya ushirikiano kati ya sehemu za Beijing, Tianjin na Hebei na kupokea shughuli zisizo za mji mkuu za Beijing."

  Wakati China ilipopanga na kujenga eneo jipya la Xiong'an, imezingatia sana uhifadhi wa mazingira, teknolojia ya hali ya juu ya kidijitali na maendeleo ya uvumbuzi, ili kujenga eneo la vielelezo linalofuata mtizamo mpya wa maendeleo. Wataalamu wanaona kuwa, ujenzi wa eneo hilo ni mpango wa muda mrefu na mkakati wa kitaifa wa China, na utatoa uzoefu kwa ajili ya ujenzi wa miji mingine katika siku za baadaye.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako