• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Russia yafanikiwa kufanya jaribio la mfumo mpya wa kisasa wa kupambana na makombora

  (GMT+08:00) 2018-04-02 18:50:28

  Jeshi la Russia limefanikiwa kufanya jaribio la mfumo mpya wa kisasa wa kupambana na makombora nchini Kazakhastan.

  Gazeti la kijeshi la Krasnaya Zvezda limemnukuu Naibu kamanda wa ulinzi wa makombora na anga wa kikosi cha anga Andrey Prikhodho akisema, mfumo mpya wa kisasa wa kupambana na makombora umefanikiwa kupiga shabaha kwa wakati uliopangwa.

  Gazeti hilo pia limesema kuwa mfumo huo, ambao umewekewa mfumo wa mawasiliano ya kijeshi umetengenezwa ili kuilinda Russia dhidi ya mashambulizi ya anga na anga za juu, pia kushughulikia mfumo wa kutoa tahadhari kwa mashambulizi ya makombora na kudhibiti anga za juu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako